Date:
21-06-2025
Reading:
1 Petro1:1-2
Utatu Mtakatifu;
Jumamosi asubuhi tarehe 21.06.2025
1 Petro 1:1-2
1 Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni katika Ponto, na Galatia, na Kapadokia, na Asia, na Bithinia;
2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Mungu mmoja;
Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;
Asubuhi hii tunamsoma Petro akitoa salamu kama utangulizi wa waraka wake kwa watu wote. Petro anawaombea watu wote neema na amani kuongezeka kwao, wakikaa katika Mungu Baba aliyetangulia kuwajua na kuwatakasa kwa Roho Mtakatifu, na kumtii Kristo kama walivyopokea Injili.
Salamu ya Petro inaakisi Utatu wa Mungu Mtakatifu! Anamtaja Baba aliyewajua watu wake. Anamtaja Yesu Kristo aliyewaokoa wanadamu kwa damu yake. Lakini pia anamtaja Roho Mtakatifu awatakasaye wote waaminio. Kwa tafakari ya juma hili, Petro anawausia wasomaji wake kumwamini Mungu wa Utatu. Kumbe nasi tudumu katika Mungu wa Utatu, yaani Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, hii ndiyo kweli. Amina
Jumamosi njema
Heri Buberwa