Date: 
23-06-2025
Reading: 
Waefeso 4:1-4

Jumatatu asubuhi tarehe 23.06.2025

Waefeso 4:1-4

1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;

2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;

3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.

Tuyashike sana maungamo yetu;

Mtume Paulo anawaandikia Waefeso juu ya umoja katika mwili wa Kristo. Paulo anawasihi watu wa Efeso kuenenda katika wito wao kwa unyenyekevu, upole, uvumilivu na upendo. Zaidi ya hapo anawasihi kuwa na umoja katika kifungo cha amani. Anawasisitizia kudumu katika tumaini moja la wito wao katika Mungu mmoja kama walivyoitwa.

Ujumbe wa Mtume Paulo kuhusu umoja katika Kristo unakuja kwetu asubuhi hii, ukitukumbusha kukaa pamoja kama kundi la Kristo. Kama Paulo anavyowaambia Waefeso, sisi kama kundi la waaminio ni mwili wa Kristo, kwa sababu sisi sote tunamwamini Kristo huyo huyo. Tukikaa pamoja katika Kristo tunakuwa wamoja, kwenye Kanisa moja, na Kristo anahubiriwa kwa urahisi kwa sababu tunapanga na kufanya pamoja. Waishio pamoja kwa upendo ni wake Kristo. Amina

Uwe na wiki njema

 

Heri Buberwa