Jumatano asubuhi tarehe 13.08.2025
Mathayo 19:16-22
16 Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele?
17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
18 Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo,
19 Waheshimu baba yako na mama yako, na, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
20 Yule kijana akamwambia, Haya yote nimeyashika; nimepungukiwa na nini tena?
21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze ulivyo navyo, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Uchaguzi wa busara;
Asubuhi hii tunasoma juu ya mtu mmoja aliyemwendea Yesu akimuuliza afanye nini ili aurithi uzima wa milele. Alionekana kuzijua amri zote, maana Yesu alipomtajia hizo amri akaonekana kuzishika tangu utoto wake. Yesu ndipo akamwambia ili kuwa mkamilifu akauze vyote alivyokuwa navyo, kisha amfuate. Yule ndugu aliondoka kwa huzuni kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Yule ndugu alishindwa kuchagua katika ya mali na kumfuata Yesu. Inaonekana aliona atapoteza mali. Lakini bila shaka, naamini angeamua kufanya alivyoelekezwa, Yesu aliijua hatma yake. Kwa maisha yetu leo, tunaalikwa kumchagua Yesu Kristo, kwa maana ya maisha tunayoishi kutotutoa kwa Yesu. Katika yote tufanyayo, busara ni kuchagua kukaa na Yesu tukimtanguliza katika yote, yeye aliye hatma yetu. Amina
Heri Buberwa Nteboya