Date: 
04-12-2025
Reading: 
Nahumu 1:9-14

Hii ni Advent 

Alhamisi asubuhi tarehe 04.12.2025

Nahumu 1:9-14

9 Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.

10 Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunyweshwa kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu.

11 Ametoka mmoja kwako, aniaye mabaya juu ya Bwana, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.

12 Bwana asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.

13 Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako.

14 Tena Bwana ametoa amri katika habari zako, ya kwamba asipandwe tena mtu awaye yote mwenye jina lako; toka nyumba ya miungu yako nitakatilia mbali sanamu ya kuchora, na sanamu ya kuyeyusha; nitakufanyia kaburi lako; kwa maana u mbovu.

Bwana mwenye haki analijia Kanisa lake;

Sura ya kwanza ya unabii wa Nahumu ni maelezo ya nguvu ya Mungu na haki. Unabii huu ulikuwa onyo kwa watu wa mji wa Ninawi ambao siku zote walikuwa maadui na waonevu wa Israeli, lakini pia tumaini kwa watu wa Yuda waliokuwa wakiteswa na Waashuru wa mji wa Ninawi. Mungu anaonesha kuangalia watu wote, wanaotesa na wanaoteswa, kila mmoja anampa haki yake.

Kuanzia mstari wa 12 Bwana anatoa tumaini kwa Yuda kwamba hawatateswa tena. Hii ilikuwa ahadi ambayo ilitosha kwa wao kumtumaini Bwana. Kumbe katika maisha tunayoishi hatuna haja ya kuogopa, maana ahadi ya Bwana kuwa nasi hudumu daima. Tuendelee kumtumaini yeye, ili akirudi tuingie uzimani. Amina

Alhamisi njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com