Date: 
05-12-2025
Reading: 
Yohana 18:36-37

Hii ni Advent 

Ijumaa asubuhi tarehe 05.12.2025

Yohana 18:36-37

36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa.

37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.

Bwana mwenye haki analijia Kanisa lake;

Asubuhi hii tunasoma Yesu akiwa mbele ya Pilato, anashtakiwa kabla ya kusulibiwa. Pilato anamuuliza kama yeye ni Mfalme, Yesu anamjibu kwamba yeye ni Mfalme, na ufalme wake siyo wa dunia hii. Inaonekana jibu la Yesu lilimsumbua sana Pilato, maana alirudia tena kuuliza swali kama Yesu ni mfalme, Yesu akamjibu "wewe wasema".

Waliomshtaki Yesu walikerwa sana na Yesu kujiita Mfalme, lakini hawakuelewa ufalme wa Yesu ulikuwaje. Yesu alidhihirika baadaye kama mfalme alipohimili mateso akafa na kufufuka, japokuwa bado wapo ambao hawakuamini hata sasa wanamsubiri Mesiya. Kumbe Yesu alikuwa Mfalme, tena Mfalme wa amani kama alivyotabiriwa. Kuita watu wote waokolewe bila gharama yoyote ila kuamini tu ni Ufalme kamili. Tumwamini Mfalme huyu ili atupe mwisho mwema. Amina

Ijumaa njema

 

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com