Date: 
06-12-2025
Reading: 
Isaya 26:11-15

Hii ni Advent 

Jumamosi asubuhi tarehe 06.12.2025

Isaya 26:11-15

11 Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

12 Bwana, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.

13 Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.

15 Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

Bwana mwenye haki analijia Kanisa lake;

Somo la asubuhi ya leo ni unabii wa Isaya kwamba mkono wa Bwana utakuwa juu ya Taifa lake daima, atawapa amani na kubariki kazi zao. Isaya anatabiri msaada kutoka kwa Mungu peke yake kwa ajili ya watu wake. Isaya anakazia ulinzi wa Mungu kwa kuwapoteza maadui na kuwaangamiza, kupoteza utambulisho wao pia. 

Tunachoona kwenye unabii wa Isaya ni upendo wa Mungu kwa watu wake. Ni kwa upendo huo alimtoa Yesu kufa msalabani kwa ajili yetu, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Uzima wa milele upo kwa ajili yetu, tukimwamini na kumfuata Yesu kwa njia ya neno lake. Jiandae kumpokea. Amina

Jumamosi njema

Heri Buberwa Nteboya 

0784 968650 

bernardina.nyamichwo@gmail.com