Date:
28-01-2026
Reading:
Ufunuo wa Yohana 22:18-21
Jumatano asubuhi tarehe 28.01.2026
Ufunuo wa Yohana 22:18-21
18 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
19 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.
21 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.
Yesu ajidhihirisha katika utukufu wake;
Somo la leo asubuhi ni mwisho wa Ufunuo wa Yohana, ambapo lipo hitimisho na baraka. Baada ya Ufunuo wake wote, Yohana anasema atakayeongeza lolote katika kitabu hiki Mungu atamuongezea mapigo. Na atakayeondoa lolote Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima. Yohana anahitimisha kwa kuonesha kuwa Yesu atarudi, anawatakia wasomaji wake neema ya Bwana Yesu.
Msisitizo wa Yohana ni kuushika ufunuo ambao alipewa na Kristo akiwa kisiwani Patmo. Kwa leo naweza kusema ujumbe muhimu ni kukishika neno la Mungu ambalo kupitia kwalo Yesu anajifunua kwetu. Neno la Mungu hatuwezi kuliongeza wala kulipunguza, bali kwa kulitii na kumcha Bwana tutaurithi uzima wa milele. Amina
Siku njema
Heri Buberwa
