Date: 
24-05-2025
Reading: 
Zaburi 144:1-4

Hii ni Pasaka

Jumamosi asubuhi tarehe 24.05.2025

Zaburi 144:1-4

[1]Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, 

Anifundishaye mikono yangu vita, 

Vidole vyangu kupigana.

[2]Mhisani wangu na boma langu, 

Ngome yangu na mwokozi wangu, 

Ngao yangu niliyemkimbilia, 

Huwatiisha watu wangu chini yangu.

[3]Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue? 

Na binadamu hata umwangalie?

[4]Binadamu amefanana na ubatili, 

Siku zake ni kama kivuli kipitacho.

Kila mwenye pumzi amsifu Bwana;

Somo la asubuhi hii ni Sala ya Daudi akiomba ukombozi na usalama wa Taifa la Mungu. Anamtaja Bwana kama ngome na Mwokozi, akimuita kuwatawanya wote walio kinyume na Taifa lake.

Daudi anapomuita Bwana kuliponya Taifa lake, anatukumbusha kumuita Bwana kuwa nasi wakati wote, maana ndiye awezaye kutufanya tuwe salama, tukidumu katika wokovu. Amina

Jumamosi njema

 

Heri Buberwa