Date:
18-06-2025
Reading:
1Yohana 5:7-10
Utatu Mtakatifu;
Jumatano asubuhi tarehe 18.06.2025
1 Yohana 5:7-10
7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.
8 Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja.
9 Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
10 Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
Mungu mmoja;
Baba, Mwana na Roho Mtakatifu;
Ni ushuhuda wa Yohana kuhusu Yesu kama mwana wa Mungu. Katika kumshuhudia Yesu huko, anamtaja Mungu mmoja ambaye yuko katika Utatu, akisema hawa watatu ni umoja. Ushuhuda huu Yohana anasema ni wa kweli, maana ni ushuhuda wa Mungu mwenyewe. Yaani kushuka kwa Yesu duniani kuokoa mwanadamu, na Roho Mtakatifu aliyeshuka kuwa mtakasaji wa roho zetu, bila kusahau uumbaji wa Baba, huu ni ushuhuda kamili.
Kwa mujibu wa Yohana, ushuhuda wa Mungu mmoja katika Utatu unakamilika kwa Imani. Yaani tukimwamini tunakuwa na ushuhuda. Tusipoamini tunamfanya kuwa mwongo, maana tunakuwa hatujaamini ushuhuda utokao kwa Mungu mwenyewe. Imani katika Mungu mmoja ndiyo itupayo ushuhuda wa kweli katika Bwana. Tusiiache Imani hii daima. Amina
Jumatano njema
Heri Buberwa